النبإ
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ ١ عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلْعَظِيمِ ٢ ٱلَّذِى هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ٣ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ٤ ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ٥
{1 - 5} Yaani, je, wanauliza hao wanaokadhibisha ishara za Mwenyezi Mungu juu ya kitu gani? Kisha akaeleza waliyokuwa wakiulizana juu yake, akasema: "Kuhusu ile habari kuu. Ambayo kwayo wanahitalifiana" kwa muda mrefu kwa namna ya kuikadhibisha na kuona kwamba ni jambo lisilowezekana. Lakini ni habari isiyokubali shaka yoyote, lakini wale wanaokadhibisha kukutana na Mola wao Mlezi hawaamini, hata ikiwafikia kila Ishara, mpaka waione adhabu chungu, na ndiyo maana akasema: "La! Karibu watakuja jua. Tena la! Karibu watakuja jua" itakapowashukia adhabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikadhibisha siku "watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu" na waambiwe, "Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukanusha!"