النبإ
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
رَّبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلرَّحْمَـٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ٣٧ يَوْمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ٣٨ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا ٣٩
{37 - 39} Yaani Yule aliyewapa vipawa hivi ndiye Mola wao Mlezi, "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" aliyeziumba na kuziendesha. "Arrahman (Mwingi wa rehema)" ambaye rehema zake zimekienea kila kitu. Aliwalea, akawarehemu na akawafanyia upole mpaka wakapata yale waliyopata. Kisha akataja ukubwa wake na mamlaka yake makubwa Siku ya Kiyama, na kwamba viumbe vyote vitanyamaza siku hiyo na havitasema na "hawatamiliki usemi mbele yake. Ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu." Kwa hivyo, hatasema yeyote ila kwa masharti haya mawili: ya kwamba Mwenyezi Mungu amemruhusu kusema, na kwamba anayosema yawe ni sawa. Kwa sababu "Hiyo ndiyo Siku ya haki" ambayo haitaenea batili ndani yake wala uwongo hautafaidisha kitu. Na katika siku hiyo "Roho atasimama" naye ni Jibril, amani imshukie, ambaye ndiye mbora zaidi wa Malaika wote. "Na Malaika" pia watasimama "kwa safu" huku wamemnyenyekea Mwenyezi Mungu, bila ya kusema lolote ila kwa idhini yake. Basi alipotia moyo na akaogopehsa, na akatoa bishara njema na akaonya. Akasema: "Basi anayetaka, na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi." Yaani, matendo mema aliyotanguliza atakayoyarudia Siku ya Kiyama.