انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المرسلات
السورة ٧٧

المرسلات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٤١–٤٥

إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى ظِلَـٰلٍ وَعُيُونٍ ٤١ وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ ٤٢ كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ٤٣ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ٤٤ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ٤٥

{41 - 45} Alipotaja adhabu ya wale wanaokadhibisha; akataja malipo ya wale wafanyao wema, akasema: "Hakika wacha Mungu" wakajiepusha kukadhibisha, wale wanaosifa na kusadiki katika kauli zao, vitendo vyao na matendo yao, na wao hawawi hivyo ila kwa kutekeleza wajibu na kuacha haramu, "watakuwa katika vivuli" vitokanavyo na wingi wa aina mbali mbali nzuri za miti inayochanua maua, "na chemichemi" itokayo katika salsabil, na kinywaji safi na vitu vinginevyo. "Na matunda wanayoyapenda" na wataambiwa: "Kuleni na kunyweni" kutokana na vyakula vitamu na vinywaji vitamu, "kwa furaha" bila ya kumsumbuliwa wala kukerwa, na furaha yake haiwezi kukamilika mpaka chakula chake na kinywaji vyake visalimike viondolewe na kila balaa na upungufu, na mpaka wahakikishe kutokana na balaa na mapungufu. "Kwa yale mliyokuwa mkiyatenda" matendo yenu ndiyo sababu iliyokupelekeni kwenye Pepo zenye neema ya kudumu, na kadhalika kila anayefanya wema katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, na akawafanyia wema waja wa Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana akasema: "Hakika ndiyo kama hivyo tunavyowalipa watendao mema. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!" Na lau kuwa haikuwa kwamba adhabu hii haina chochote isipokuwa kukosa neema hii, basi hilo lingetosha kuwa huzuni na kunyimwa.