انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المرسلات
السورة ٧٧

المرسلات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٩–٣٤

ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ٢٩ ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ ظِلٍّ ذِى ثَلَـٰثِ شُعَبٍ ٣٠ لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِى مِنَ ٱللَّهَبِ ٣١ إِنَّهَا تَرْمِى بِشَرَرٍ كَٱلْقَصْرِ ٣٢ كَأَنَّهُۥ جِمَـٰلَتٌ صُفْرٌ ٣٣ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ٣٤

{29 - 34} Hii ni moja ya adhabu kali iliyotayarishwa kwa ajili ya wahalifu wanaokadhibisha kwamba wataambiwa Siku ya Kiyama: "Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha!" Kisha akaeleza hayo kwa kusema "Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!" Yaani, nendeni kwa kivuli cha moto wa Jahannamu, ambao umegawanyika matawi matatu. Kivuli hicho. "Hakikingi moto" kwani humo hamna faraja wala utulivu. "wala hakiwaepushi" mwenye kukaa humo "kutoka na mwako." Bali miali ya moto huo itamzunguka kulia na kushoto na pande zote; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Yatawekwa juu yao mat'abaka ya moto, na chini yao matabaka." Na akasema "Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu." Kisha akataja ukubwa wa cheche za moto huo, ambazo zinaonyesha ukuu wake, utisho wake, na mandhari yake mabaya. Akasema, "Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano." Hili linaashiria kuwa moto huo una giza katika miali yake, makaa yake na cheche zake, na kwamba ni mweusi, wa kuchukiza sana katika mandhari yake, wenye moto mkali sana. Tunamuomba Mwenyezu Mungu salama kutokana nao, na kutokana na matendo yanayomweka mtu karibu nao. "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!"