المدثر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَمَا لَهُمْ عَنِ ٱلتَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ ٤٩ كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ ٥٠ فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍۭ ٥١ بَلْ يُرِيدُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ٥٢ كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ ٥٣
{49 - 53} Mwenyezi Mungu alipobainisha hatima ya wale waliohalifu kitambo na akabainisha watakachofanyiwa, akawaelekezea hawa waliopo makaripio na lawama, akasema: "Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?" Yaani, wanaupinga na na wameghafilika mbali nao. "Kama kwamba wao" katika kuukimbia kwao mno "ni mapunda waliotimuliwa." Basi wakakimbizana wao kwa wao, kwa hivyo wakazidi kukimbia. "Wanaomkimbia simba" au mwindaji na mpiga mishale anayewataka. Na hali hii ndiyo aina mojawapo kubwa zaidi ya kujiweka mbali na haki, lakini pamoja na kujiweka mbali huku na kupeana mgongo, wanadai madai makubwa. "Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa" zimshukie kutoka mbinguni. Anadai kwamba hajisalimishi kwa haki Isipokuwa kwa hilo. Lakini wamesema uwongo. Kwani lau ingewafikia kila ishara, hawangeamini mpaka waione adhabu chungu. Kwa sababu ziliwajia ishara zilizo wazi zinazobainisha na kuiweka wazi haki. Basi ikiwa kulikuwa na wema ndani yao, wangeamini, na ndiyo maana akasema: "Hasha!" Yaani, hatuwapi kile walichokiomba, kwani hawakukusudia kwa hilo isipokuwa kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ameshindwa. "Kwani wao hawaiogopi Akhera?" Kwa sababu wangekuwa wanaiogopa, hawangefanya hayo waliyoyafanya.