الجن
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَنَّا لَمَسْنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدْنَـٰهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا ٨ وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَـٰعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ ٱلْـَٔانَ يَجِدْ لَهُۥ شِهَابًا رَّصَدًا ٩
{8 - 9} "Nasi tulizigusa mbingu." Yaani, tulizijia na kuzifanyia mtihani, "na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu" wanaozuia kufikia pande zake na hata kuzikaribia. Na vilikuwepo "vimondo" ambavyo hupigwa kwavyo wanaosikiliza kwa siri, na hili ni kinyume na desturi yetu ya hapo mwanzo. Kwani tulikuwa tunaweza kuzifikia habari za mbinguni, basi "tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza" na tungekusanya kutoka katika habari za mbinguni anachotaka Mwenyezi Mungu. "Lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia" na kilichotayarishwa kumharibu na kumteketeza. Na hili lilikuwa kwa sababu ya jambo kubwa na habari kubwa. Basi wakawa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu alitaka kufanya tukio kubwa litokee duniani, la uzuri au ubaya. Ndiyo maana wakasema: