الحاقة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ٢١ فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ٢٢ قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ ٢٣ كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَآ أَسْلَفْتُمْ فِى ٱلْأَيَّامِ ٱلْخَالِيَةِ ٢٤
{21 - 24} "Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza." Yaani, yanayokusanya yale yanayotamaniwa na nafsi na yale ambayo macho yanayafurahia, na tayari waliridhika nayo na wala hawataki kuchagua chochote badala yake. "Katika Bustani ya juu" Yaani: nyumba na majumba yaliyoinuka juu sana. "Matunda yake yakaribu." Yaani matunda yake ni miongoni mwa aina za matunda yaliyo karibu na yaliyo mepesi sana kwa watu wake kuyachuma huku wakiwa wamesimama, wamekaa, na wameegemea, na wataambiwa kwa heshima: "Kuleni na mnywe" kutoka katika kila chakula kitamu na kinywaji kitamu, "kwa furaha" kikamilifu bila ya kero wala usumbufu wowote. Na mlipewa malipo hayo "kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita" miongoni mwa matendo mema - na kuacha matendo maovu - kama vile Swala, saumu, sadaka, Hijja, kuwafanyia mema viumbe, kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumgeukia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu aliyafanya matendo kuwa ni sababu ya kuingia katika bustani za mbinguni, na kiini cha furaha yake, na msingi wa furaha yake.