انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · القلم
السورة ٦٨

القلم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨

فَلَا تُطِعِ ٱلْمُكَذِّبِينَ ٨

{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - "Basi usiwatii wanaokadhibisha." Wale waliokukadhibisha na wakaipinga haki; kwani hawastahili kutiiwa; kwa sababu hawaamrishi isipokuwa yale yanayoafikiana na matamanio yao tu, nao hawataki isipokuwa batili. Kwa hivyo, mwenye kuwatii, anaendea mambo yenye yatakayomdhuru. Na hili ni la jumla katika kila mwenye kukadhibisha, na katika kila utiifu unaotokana na kukadhibisha, hata kama muktadha huu uko katika jambo maalumu, ambalo ni kwamba washirikina walimuuliza Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anyamaze na aache kuikashifu miungu yao na dini yao.