القلم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَـٰوَمُونَ ٣٠ قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَـٰغِينَ ٣١ عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ ٣٢
{30 - 32} Na kwa sababu ya hilo wakajuta sana, na wakageukiana "kulaumiana wao kwa wao" juu ya yale waliyoyafanya. "Wakasema: 'Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka'" katika haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya waja wake. "Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi." Basi wakataraji Mwenyezi Mungu atawapa kilicho bora kuliko hilo, na wakaahidi kwamba watamrudia mno Mwenyezi Mungu na kusisitiza juu ya hilo katika dunia hii. Kwa hivyo, ikiwa wako kama walivyosema, basi linaloonekana ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwabadilishia mahali pake kilicho bora zaidi yake katika dunia hii. Kwa sababu anayemwomba Mwenyezi Mungu kwa ukweli, akamtaka sana na kumtaraji, atampa ombi lake.