الطلاق
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَـٰلِغُ أَمْرِهِۦ ۚ قَدْ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَىْءٍ قَدْرًا ٣
{3} Na kauli yake: "Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu" katika mambo ya dini yake na mambo yake ya kidunia, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kumletea yenye kumanufaisha na kumuepusha mbali na yenye kumdhuru, na akawa na imani naye katika kuyasahilisha hayo, basi "Yeye humtosha." Yaani, atamtosha katika jambo alilomtegemea ndani yake. Na ikiwa jambo liko chini ya Mkwasi, Mwenye nguvu, Mshindi, Mwingi wa kurehemu, basi Yeye yuko karibu na mja kuliko kitu kingine chochote. Lakini labda hekima ya kimungu ikahitaji kulichelewesha hadi wakati ufaao kwake. Kwa ajili hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake." Yaani, mipango yake na hukumu zake zitekelezeke, lakini amekifanyia "kila kitu na kipimo chake" ambao hakiuvuki wala kukipunguza.