الجمعة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى بَعَثَ فِى ٱلْأُمِّيِّـۧنَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا۟ مِن قَبْلُ لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ ٢
{2} "Yeye ndiye aliyemtuma Mtume kwenye watu wasiojua kusoma na kuandika." Maana yake wasiojua kusoma na kuandika ni wale wasio na kitabu chochote wala alama ya utume miongoni mwa Waarabu na wengineo miongoni mwa Watu wa Kitabu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawapa neema kubwa kuliko neema aliyowapa wengineo. Kwa sababu wao hawakuwa na elimu na heri, na walikuwa katika "upotofu ulio dhahiri." Walikuwa wakiabudu masanamu, miti na mawe, na walikuwa na tabia za wanyama mwitu, ambapo wanyonge wao walikuwa wakiliwa na wenye nguvu wao. Na walikuwa katika ujinga mkubwa mno bila kujua elimu za Manabii. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia Mtume kutokana nao wenyewe, ambaye wanajua nasaba yake, sifa zake nzuri, na ukweli wake, na akamteremshia Kitabu chake, "ili awasomee Aya zake" zenye kukata, zenye kuwalazimu waamini na wawe na yakini. "Na awatakase" kwa kuwabainishia kwa kina maadili mema, na kuwahimiza kushikamana nao, na kuwakemea kutokana na tabia mbaya, "na awafunze Kitabu na hekima." Yaani, elimu ya Kitabu (Qur-ani) na Sunna, ambayo inajumuisha elimu za watu wa kale na za wa mwisho. Kwa hivyo, wakawa baada ya kufundishwa huku na kutakaswa huku miongoni mwa viumbe wajuao zaidi. Bali walikuwa waongozi wa wenye elimu, dini na wenye maadili makamilifu zaidi katika viumbe vyote, na wabora wao zaidi katika uwongofu na heshima, wao wenyewe waliongoka na pia wakawaongoza wengine, basi wakawa ni maimamu wa waongofu na viongozi wa wacha Mungu. Basi Mwenyezi Mungu ni mwenye neema kamili zaidi na zawadi tukufu zaidi kwao kwa kuwatumia Mtume huyu.