انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصف
السورة ٦١

الصف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨

يُرِيدُونَ لِيُطْفِـُٔوا۟ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفْوَٰهِهِمْ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَـٰفِرُونَ ٨

{8} Ndiyo maana [Mwenyezi Mungu] akasema juu yao: “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao” Yaani: kwa sababu ya kauli za upotovu wanazozitoa ambazo kwazo wanaikanusha haki, ilhali hazina uhakika wowote, bali zinamzidishia mwenye kuona elimu kuhusu uongo batili wanayoifanya. “Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.” Yaani, Mwenyezi Mungu ameshachukua dhamana kuinusuru dini yake, na kuitimiza haki aliyowatuma nayo Mitume wake, na kuifanya nuru yake ionekane katika nchi zote, hata kama makafiri watachukia, na kwa sababu ya kuichukia wakatoa kila wawezalo miongoni mwa yale wanayoyatumia kufikia kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana watashindwa, na mfano wao ni kama mtu anayepuliza jua kwa kinywa chake ili kulizima. Kwa hivyo, hawakufanikiwa kufikia kile walichotaka, wala akili zao hazikusalimika kutokana na upungufu na kashfa.