الممتحنة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّا يَنْهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ لَمْ يُقَـٰتِلُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَـٰرِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوٓا۟ إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُقْسِطِينَ ٨
{8} Na zilipoteremshwa Aya hizi tukufu zenye kuwashawishi kuwafanyia uadui makafiri, ziliwaathiri Waumini sana, nao wakafanya walivyoamrishwa kikamilifu zaidi, na hata wakaona kwamba ni dhambi kuwaunga baadhi ya jamaa zao washirikina, na wakadhania kuwa hilo linajumuishwa katika yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu akawaambia kuwa haya hayakujumuishwa katika yale aliyoyaharamisha, akasema: “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” Yaani, Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwa wema, kuwaunga, na kuwalipa washirikina miongoni mwa jamaa zenu na wengineo kwa wema na uadilifu. Walikuwa katika hali ambayo hawawezi kusimama imara kupigana nanyi kwa ajili ya dini yenu na kuwatoa majumbani mwenu. Basi hakuna dhambi juu yenu mkiwaunga; kwa manaa kuwaunga katika hali hii hakujakatazwa wala hakuna lawama. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu wazazi makafiri ikiwa mtoto wao ni Mwislamu: “Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani.”