انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٨

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ٩٨

{98} "Na Yeye ndiye aliyewaanzisha kutokana na nafsi moja;" naye ni Adam, amani iwe juu yake. Mwenyezi Mungu alianzisha kutoka kwake kitu hii sampuli ya kibinadamu ambayo iliijaza ardhi, na haijaacha kuzidi na kukua. Ambayo ametofautiana katika maadili yake, maumbile yake, na sifa zake kutofautiana ambako haiwezekani kuudhibiti, wala haifikiwi kuueleza.Na mwenyezi Mungu akawafanyia pahali pa kutulia. Yaani, mwisho wanaoufikia na marejeo wanayopelekwa kwayo. Nayo ni Nyumba ya kudumu ambayo hakuna pahali pengine pa kutulia pasipokuwa hapo, wala hakuna utulivu mwisho juu yake. Basi Nyumba hii ndiyo Nyumba ambayo viumbe viliumbwa ili vikae hapo, na wakawekwa katika dunia hii ili wajitahidi katika sababu zake ambazo inaanzishwa juu yake na inaimarishwa kwayo. Na Mwenyezi Mungu aliwaweka katika migongo ya baba zao na matumbo ya uzazi ya mama zao, kisha katika nyumba ya dunia, kisha katika Barzakh; yote hayo ni kwa jina la amana ambayo haitulii wala kukaa imara. Lakini inahamishwa kutoka humo, mpaka ifikishwe kwenye nyumba ambayo ndiyo pahali pa kutulia. Na ama nyumba hii; hiyo ni mahali pa kuhifadhi tu, na njia ya kupita. "Hakika, tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaofahamu" kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aya zake, na wanafahamu kutoka kwake hoja zake na ushahidi wake ulio wazi.