انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٢

وَهَـٰذَا كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ٩٢

{92} Yaani, "na hiki" (kitabu cha) Qur-aani ambacho "tulikiteremsha" kwako "kilichobarikiwa;" yaani sifa yake ni kwamba kimebarikiwa. Na hilo ni kwa sababu ya wingi wa heri zake, na wingi wa wema wake { chenye kusadikisha yale yaliyokitangulia. Yaani, chenye kuafikiana na Vitabu vilivyotangulia, na chenye kushuhudia ukweli wake, "na ili uuonye Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake." Yaani, pia tulikiteremsha ili uuonye Mama wa Miji - nayo ni Makka Al-Mukarramah - na wale walio pembezoni mwake miongoni mwa nchi za Waarabu, na hata katika nchi nyingine zote; ili uwaonye watu adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kuchukua kwake umma mbalimbali, na uwaonye dhidi ya yale yanayosababisha hayo. "Na wale wanaoiamini Akhera wanakiamini." Kwa sababu hofu inapokuwa katika moyo, nguzo zake zinaimarika na kufuata yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu; "nao wanazihifadhi Swala zao." Yaani, wanadumu juu yake na wanazihifadhi nguzo zake, na mipaka yake, na masharti yake, na adabu zake, na yale yote yenye kuikamilisha. Mwenyezi Mungu atufanye tuwe miongoni mwao.