الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِسْمَـٰعِيلَ وَٱلْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ ٨٦
{86} "Na Ismail" mwana wa Ibrahim, baba wa taifa ambalo ndilo taifa bora zaidi, nalo ni taifa la Kiarabu, na baba wa bwana wa mwana wa Adam Muhammad - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani. "Na Yunus" bin Mata, "na Lut’" bin Harun, kaka yake Ibrahim, "na kila mmoja wao" katika hawa Manabii na Mitume; "tulimfadhilisha juu ya walimwengu wote." Kwa sababu daraja za fadhila ni nne. Nazo ni zile alizotaja Mwenyezi Mungu kwa kauli yake, "Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao wako pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema." Basi hawa wako katika daraja la juu, bali wao ndio Mitume bora zaidi kuliko wote. Kwa maana Mitume ambao Mwenyezi Mungu alitusimulia katika Kitabu chake bila ya shaka ndio bora zaidi kuwaliko wale ambao hakutusimulia habari yao.