الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْرِفُونَهُۥ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَآءَهُمُ ۘ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ٢٠
{20} Alipofafanua ushahidi wake na ushahidi wa Mtume wake juu ya upweke wake, na ushahidi wa washirikina ambao hawana elimu juu ya kinyume chake, akataja kuwa Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, "wanalijua hilo." Yaani, wanajua usahihi wa upweke wake, "kama wanavyowajua watoto wao;" yaani, hawana shaka yoyote katika hilo kwa namna yoyote, kama vile hawachanganyiki kuhusu watoto wao, hasa watoto wao wa kiume ambao wanaandamana aghalabu na baba zao. Na inawezekana kwamba kivumishi (katika wanamjua) kunamrejelea Mtume Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - na kwamba, Watu wa Kitabu hawachanganyiki kuhusu usahihi wa ujumbe wake wala hawautilii shaka kwa sababu ya bishara njema walizo nazo juu yake na sifa zake ambazo zinamwingia yeye tu, na wala hazimfailii asiyekuwa yeye. Na maana hizo mbili zinaambatana. Kauli yake, "Wale waliozihasiri nafsi zao;" yaani, walizikosesha kile zilizoumbiwa, miongoni mwa imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na wakaziharamishia fadhila ya ufalme wenye heshima, "basi wao hawaamini." Kwa hivyo, ikiwa haikupatikana imani kutoka kwao, basi usiulize juu ya hasara na uovu ambao unawapata.