الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَهُوَ ٱلْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ ١٨
{18} "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu za ushindi juu ya waja wake," basi hakuna hata mmoja katika wao awezaye kufanya kitu, hakuna mwenye kusonga awezaye kusonga, wala hatulii mwenye kutulia isipokuwa kwa kutaka kwake, na wafalme na wengineo hawawezi kutoka katika ufalme wake wala mamlaka yake. Bali wao huendeshwa, wametiwa katika nguvu zake za ushindi. Basi ikiwa yeye ndiye Mwenye nguvu za ushindi, na wengineo wametiwa chini ya nguvu zake za ushindi, basi yeye ndiye Anayestahiki kuabudiwa. "Na Yeye ndiye Mwenye hekima" katika yale Aliyoyaamrisha na kuyakataza, na akalipa thawabu na akaadhibu, na katika aliyoyaumba na kuyakadiria "Mwenye habari zote;" Mwenye kujua siri na dhamiri na yaliyofichika ya mambo yote. Na yote haya ni katika ushahidi wa upweke wake.