الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ أَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْغِى رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَىْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ١٦٤
{164} "Sema: "Je nimtafute Mola Mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu" miongoni mwa viumbe. Yaani, je ni zuri hilo, na inanifailia kwamba nimchukue asiyekuwa Yeye kuwa ndiye Mlezi na Mwendesha mambo, na Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Basi viumbe vyote viko chini ya Umola Wake, na vinaifuata amri Yake. Kwa hivyo ikawa ni wajibu kwangu na wengineo kumchukua Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola Mlezi na amridhie, na kwamba asifungamane na yeyote miongoni mwa wanaolelewa, wenye mahitaji, wasio na uwezo. Kisha akatia moyo, na akahofisha kwa malipo hayo, akasema, "Na wala haichumi kila nafsi" katika heri na uovu "isipokuwa ni juu yake." Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Mwenye kutenda mema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, ni juu yake mwenyewe." "Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine." Bali kila mmoja ni juu yake mzigo wa nafsi yake. Na ikiwa yeyote alisababisha kupotea kwa wengine na mzigo wake, basi ni juu yake mzigo wa kusababisha, bila ya kupunguza katika mzigo wa aliyetenda hasa. "Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu" Siku ya Qiyama. "Kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake;" ya heri na maovu. Na Atawalipa kwa hayo malipo kamili zaidi.