انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٥٩

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَرَّقُوا۟ دِينَهُمْ وَكَانُوا۟ شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِى شَىْءٍ ۚ إِنَّمَآ أَمْرُهُمْ إِلَى ٱللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ ١٥٩

{159} Yeye Mtukufu anawatishia wale walioigawanya dini yao; Yaani, waliitawanya na wakatawanyika ndani yake, na kila mmoja akajitwalia fungu katika majina ambayo hayamnufaishi mtu katika dini yake chochote. Kama vile Uyahudi, na Ukristo, na Umajusi, au haikamiliki kwayo imani yake; kwa kuchukua kitu katika Sharia na kukifanya kuwa ndiyo dini yake na kuacha mfano wake au kilicho bora zaidi yake. Kama ilivyo hali ya watu wa makundi miongoni mwa wana uzushi na upotovu, wanaougawanya umma. Na Aya hii tukufu iliashiria kuwa dini inaamrisha umoja na mfungamano, na inakataza mifarakano na kuhitilafiana baina ya watu wa dini na katika masuala yake yote ya msingi na tanzu, na kuamrisha kwake kujitenga na wale walioigawanya dini yao. Kwa hivyo akasema, "Wewe si miongoni mwao katika chochote;" yaani, wewe si katika wao na wao si katika wewe. Kwa sababu walikuhalifu na wakakupinga. "Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu," watarudishwa kwake, na atawalipa kwa vitendo vyao; "kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda."