انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٨

سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشْرَكْنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَىْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا۟ بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَآ ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ١٤٨

{148} Huku ni kujulisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba washirikina watasimamisha hoja juu ya ushirikina wao na kuharamisha kwa yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kwa Qadha (majaliwa) na Qadar (kutokea kwake). Na wanakufanya kutaka kwa Mwenyezi Mungu kunakojumuisha kila kitu miongoni mwa heri na mabaya kuwa ni hoja ya kuwazuia wao kulaumiwa. Na walisema yale aliyojulisha Mwenyezi Mungu kwamba watayasema; kama alivyosema katika Aya nyingine: "Na walisema wale walioshirikisha: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake" hadi mwisho wa Aya. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa hoja hii hawajaacha Umma mbalimbali wanaokadhibisha kuitumia kujizuia dhidi ya kulingania kwa Mitume na wanaitumia kama hoja yao, lakini haikuleta chochote ndani yao na wala haikuwanufaisha. Na haijaacha hii kuwa ndiyo tabia yao mpaka Mwenyezi Mungu akawaangamiza na akawaonjesha adhabu yake. Na ikiwa ingekuwa hoja sahihi, basi ingeliwazuia adhabu hiyo. Na Mwenyezi Mungu alipowafikishia adhabu, kwa sababu adhabu yake haimfikii isipokuwa mwenye kuistahiki, basi inajulikana kuwa ni hoja mbovu na dhana potofu katika njia nyingi: Miongoni mwake ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu kuwa lau ingekuwa ya kweli, basi adhabu haingewapata. Na miongoni mwake ni kwamba, Hoja ni lazima iwe ni hoja yenye msingi wa elimu na ushahidi. Na ama ikiwa imeegemezwa juu ya dhana tu na kukisia, ambako hakunufaishi chochote mbele ya haki, basi hiyo ni batili. Na ndiyo maana akasema, "Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo?" Na lau wangekuwa na elimu - na wao ni wapinzani wakubwa mno- wangeitoa. Na pindi hawakuitoa, ilijulikana kuwa hawana elimu yoyote. "Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu." Na mwenye kuijenga hoja zake juu ya makisio na dhana, basi yeye yuko katika batili na mwenye hasara. Basi itakuwaje ikiwa ataijenga juu ya uasi, na ukaidi, na uovu, uharibifu?