انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٢

وَمِنَ ٱلْأَنْعَـٰمِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ١٤٢

{142} Yaani, "Na" amewaanzishia "katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na kutoa matandiko" yaani, baadhi yao mnabebea juu yao na mnawapanda, na mengine hawafai kubebeshwa na kupanda juu yao kwa sababu ya udogo wao, kama vile ngamia wadogo na mfano wake, na ambao ndio Al-Farsh. Kwa hivyo, kwa mtazamo wa kubeba na kupanda, wanagawanyika katika sehemu hizi mbili. Na ama kwa mtazamo wa kula na aina nyinginezo za kufaidika, hao wote wanaliwa na kunufaika nao. Na ndiyo maana akasema: "Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani;" yaani, Njia zake na matendo yake ambayo miongoni mwayo ni nyinyi kuharamisha baadhi ya yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu. "Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi." Kwa hivyo, hawaamrishi isipokuwa yale yenye kuwadhuru na mashaka yenu ya milele.