الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَدْ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓا۟ أَوْلَـٰدَهُمْ سَفَهًۢا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا۟ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفْتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا۟ وَمَا كَانُوا۟ مُهْتَدِينَ ١٤٠
{140} Kisha akaeleza hasara yao na upumbavu wa akili zao, kwa hivyo akasema: "Hakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu." Yaani, waliihasiri dini yao, na watoto wao, na akili zao, na baada ya kuwa na akili timamu, wakawa sasa wanasifiwa kwa upumbavu mbaya na upotovu, "na wakaharimisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu." Yaani, yale Aliyoyafanya kwa kuwa rehemu, akawapa kama riziki kwao, lakini wakaukataa ukarimu wa Mola wao Mlezi, na hawakutosheka na hilo, bali wakausifu kuwa ni haramu ilhali ni miongoni mwa yale yaliyo halali zaidi. Na yote haya ni "kumzulia Mwenyezi Mungu uongo;" yaani uwongo anaodanganya kwa huo kila mkaidi, kafiri mkubwa. "Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka," yaani walikwisha potea upotovu wa mbali, na wala hawakuwa waongofu katika chochote miongoni mwa mambo yao.