الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَـٰدِهِمْ شُرَكَآؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا۟ عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ١٣٧
{137} Na miongoni mwa upumbavu wa washirikina na upotovu wao ni kwamba "Na kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina." - Yaani, viongozi wao na mashetani wao – kuwaua watoto wao. Nao ndio wale wanaowazika watoto wao kwa kuogopa umasikini, na wanawake kwa kuogopa fedheha. Na yote haya ni mbaya mno, na washirika wao hao hawajaacha kuwapambia hayo ili yawe kwao katika mambo mazuri na sifa zenye kutamanika. Na kama Mwenyezi Mungu angetaka kuwazuia na kuweka kuzuizi kati yao na vitendo vyao hivi, na kuwazuia watoto wao kuuawa na wazazi wao; basi hawangefanya hivyo. Lakini hekima yake ilihitaji kuwaacha na matendo yao, ili awazidishe kuzama katika dhambi, na kuwapa muhula, na wao kutojali hali yao. Na ndiyo maana akasema, "Basi waache na hayo wanayozua ya uwongo." Yaani, waache na uongo wao na kuzua kwao uongo, na wala usihuzunike juu yao. Kwa maana, wao kwa hakika hawatamdhuru Mwenyzi Mungu kitu.