الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَرَبُّكَ ٱلْغَنِىُّ ذُو ٱلرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِنۢ بَعْدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ ءَاخَرِينَ ١٣٣
{133} Na Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake kutenda matendo mema, na akawakataza matendo mabaya kwa kuwahurumia na kuwatakia masilahi yao. Na vinginevyo, Yeye ndiye anayejitosheleza kwa dhati yake asiyewahitaji viumbe vyake vyote. Kwa hivyo, utiifu wa mtiifu haumnufaishi, kama vile maasi ya waasi hayamdhuru. "Akitaka, atawaondoa" kwa kuwaangamiza, "na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyowatoa kutokana na dhuria ya kaumu wengine." Basi ikiwa mnajua kwamba nyinyi ni lazima mtatoka katika nyumba hii kama walivyotoka wasiokuwa nyinyi, nanyi mtaondoka humo na muiachie wale walio baada yenu kama walivyoondoka wale wa kabla yenu na wakaicha kwa ajili yenu. Basi kwa nini mliichukua kuwa mahali pa kukaa, na mkaifanya kuwa makazi, na mkasahau kuwa ni nyumba ya mapito, si nyumba ya kukaa; na kwamba mbele yenu kuna nyumba ambayo ndiyo nyumba iliyokusanya kila neema na imesalimika na kila balaa na upungufu? Nayo ndiyo nyumba wanayoifanyia juhudi wale wa mwanzo na wa mwisho, na wanaielekea wale waliotangulia na waliofuatia ambako wakipafikia, basi hapo ndipo pana kudumu na makazi ya lazima, na lengo ambalo hakuna lengo lingine zaidi yake, na lile linalotafutwa ambalo kila linalotafutwa linaishia hapo, na yale yanayohofiwa ambayo kinatoweka kila kitu kinachohofiwa isipokuwa hayo. Hapo, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuna yale yanayotamaniwa na nafsi na yale yanayopendeza macho, na wanashindana kwa ajili yake wale wanaoshindana miongoni mwa ladha za nafsi, na wingi wa furaha, furaha ya miili na mioyo, na kuwa karibu na Mwenye kuijua zaidi ghaibu. Basi na kwa jina la Mwenyezi Mungu mtu na afanye hima inayohusiana na matukufu haya, na nia inayokwenda juu hadi katika viwango vya juu zaidi. Na ni kupunjwa kupi huku kwa fungu la mwenye kuridhia yaliyo duni, na ni ya chini mno vipi hima ya mwenye kuchagua mapatano ya waliopunjwa.