الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِى ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ١٣
Jua kwamba Sura hii tukufu ilijumuisha kuisimamisha tauhidi kwa kila ushahidi wa kiakili na kimaandiko. Bali ilikuwa karibu yote kuhusiana na tauhidi tu na kuwajadili wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaomkadhibisha Mtume wake. Na katika aya hizi, Mwenyezi Mungu alitaja chenye kubainisha kwazo uongofu, na kuangamiza kwazo shirki.
{13} Basi ikataja kwamba "ni vyake" Yeye Mtukufu "vilivyotulia katika usiku na mchana" na hivyo ni viumbe vyote, kuanzia wanadamu wake, na majini yake, na Malaika wake, na wanyama wake, na visivyo na uhai vyake. Vyote hivyo ni viumbe vinavyoendeshwa, na ni waja waliotiishwa kwa Mola wao Mlezi, Mkuu, Mshindi, Mmiliki. Basi Je, ni sahihi katika akili na maandiko kwamba aabudiwe yeyote katika hao wanaomilikiwa ambao hawana manufaa kwake, wala madhara, na aachwe kufanyiwa ikhlasi Muumba, na Mwendesha mambo, Mmiliki, Mwenye madhara, na Mwenye manufaa? Au je, akili timamu na nyoofu zinaita kwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote ibada, na mapenzi, na hofu na matumaini? "Mwenye kusikia;" sauti zote pamoja na kutofautiana kwa lugha na mahitaji mbalimbali. "Mwenye kujua vyema," yale yaliyokuwa, na yale yatakayokuwa, na yale ambayo hayakuwa lau yangekuwa, yangekuwaje, Mwenye kuyajua yaliyo dhahiri na yaliyofichika.