الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ لَئِن جَآءَتْهُمْ ءَايَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا ٱلْـَٔايَـٰتُ عِندَ ٱللَّهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَآ إِذَا جَآءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ١٠٩
{109} Yaani, na waliapa washirikina waliomkadhibisha Mtume Muhammad -rehema na amani zimshukie - kwa Mwenyezi Mungu "viapo vyao vikali zaidi." Yani viapo walivyojitahiji ndani yake, na wakavisisitiza, "kwamba ikiwajia Ishara" yenye kuonyesha ukweli wa Muhammad -rehema na amani zimshukie - "bila ya shaka wataiamini." Na maneno haya ambayo yalitoka kwao, makusudio yao hayakuwa na uwongofu ndani yake bali makusudio yao yalikuwa ni kujiondolea upinzani, na kukataa yale aliyokuja nayo Mtume bila ya shaka yoyote. Kwa maana Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Mtume wake – rehema na amani ziwe juu yake – kwa Aya zilizo wazi, na ushahidi ulio wazi, ambazo pindi tu zinapozingatiwa, haibaki tuhuma yoyote ya chini kabisa, wala tatizo hata kidogo katika usahihi wa yale aliyokuja nayo. Basi ombi lao la Aya, baada ya hayo ni katika mlango wa ukaidi ambao hauhitaji jawabu; bali huenda kuacha kuwajibu ndiyo bora zaidi kwao. Kwani Mwenyezi Mungu ilikwisha pita Sunna yake katika waja wake kwamba wale wanaowapendekezea Mitume wao Aya, ikiwajia na wasiziamini, basi Yeye kwa hakika huwaharakishia adhabu. Na ndiyo maana akasema, "Sema: Hakika, Ishara hizo ziko kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, Yeye ndiye anayezituma akitaka, na anazizuia akitaka. Mimi sina chochote katika jambo hilo basi kuniomba kwenu mimi Aya ni dhuluma na ombi la kile nisichokimiliki. Lakini mnapaswa kunielekezea kufafanua yale niliyowajia nayo, na kuyasadiki, na tayari yameshafanyika. Lakini pamoja na hayo, haijulikani ikiwa zitakapowajia Ishara hizo wataziamini na kuzisadiki. Bali uwezekano mkubwa kwa yule ambaye hii ndiyo hali yake [ni kwamba], hataamini. Ndiyo maana akasema, "Na ni nini kitawajulisha kuwa zikija, hawataamini?"