الحشر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنْهُمْ فَمَآ أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُۥ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ٦
Kisha akataja wale ambao mali na vitu vyao viliwaendea, akasema: “Na mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao,” yaani kutoka kwa watu wa kijiji hiki, ambao ni Banu Nadhir. “Basi” enyi kundi la Waislamu, “hamkuikimbilia mbio kwa farasi wala ngamia.” Yaani, hamkuvipata kwa nafsi zenu wenyewe wala kwa wanyama wenu. Bali Mwenyezi Mungu aliwatia hofu kubwa mioyoni mwao, kwa hivyo vikawajia bila juhudi. Ndiyo maana akasema: “Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno juu ya kila kitu.” Kwa sababu ya utimilifu wa uwezo wake ni kwamba hakuna lisilowezekana linaloweza kukataa atakacho, wala hakuna mtu mwenye nguvu anayeweza kupata nguvu dhidi yake