المجادلة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ يُظَـٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا۟ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَآسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِۦ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ٣
{3} “Na wale wanaojitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema.” Wanachuoni walihitalifiana juu ya maana ya ‘kisha wakarudia’. Basi kuna wale waliosema kuwa ni kuweka azimio ya kumuingilia mke ambaye mtu mwenyewe alikuwa amemfananisha na mama yake, na kwamba kwa kuwa tu na azimio hilo analazimika kutoa kafara iliyotajwa hapo juu, na hili linadhihirishwa na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwamba kafara iwe kabla ya kujamiiana, na hilo linakuwa kwa kuweka azimio tu. Na ikasemwa kwamba maana yake ni kujamiiana, na hili linaashiriwa na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu alisema: “Kisha wakarudia katika yale waliyoyasema” Na yale waliyoyasema ni ngono tu. Hata hivyo, kulingana na kauli zote mbili, pindi kurudi kunapopatikana tu, inakuwa kafara ya kujiharamishia huku ni “kumkomboa mtumwa” Muumini, kama ilivyowekewa sharti hili la imani katika Aya inayohusiana na kuua. Na anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, lakini kwa sharti kwamba awe salama kutokana na kasoro zinazoweza kuathiri vibaya utendaji kazi wake, “kabla hawajagusana. Kwa hayo;” yaani, hukumu tuliyokutajieni “Mnapewa maonyo” kwa maana akikumbuka kwamba itamlazimu amwachilie huru mtumwa, bila shaka atajizuia kufanya hilo. “Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda.” Kisha atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake.