الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِۦٓ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ٩
{9} Pamoja na wema wake huu na kujali kwake, hakutosheka kwa ulinganiaji wa Mtume tu, ambaye ndiye mtukufu zaidi wa walimwengu wote. Bali alimsaidia kwa miujiza na akakuonyesheni ukweli wa yale aliyokuja nayo kwa ishara zilizo wazi. Ndiyo maana akasema: "Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi" zinazowaonyesha wale wenye wenye akili kwamba kila alichokileta ni sahihi, na kwamba ndiyo haki ya yakini. "Akutoeni" kwa kukutumieni Mtume na yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa mkono wake kama vile Kitabu na hekima "kutoka gizani kuingia kwenye nuru." Yaani, kutoka kwenye viza vya ujinga na ukafiri hadi kwenye nuru ya elimu na imani. Haya ni katika rehema na upole wake juu yenu. Ambapo aliwarehemu zaidi waja wake hata kuliko mama kwa mwanawe, "Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu."