الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَىْءٍ مِّن فَضْلِ ٱللَّهِ ۙ وَأَنَّ ٱلْفَضْلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ ٢٩
{29} Na kauli yake: "Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu." Yaani, tulikuelezeni neema zetu na wema wetu kwa wale walioamini imani ya ujumla, na wakamcha Mwenyezi Mungu, na wakamuamini Mtume wake; ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote ju ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Yaani, hawawezi kumzuilia yeyote mbali na Mwenyezi Mungu kwa matamanio yao na akili zao mbovu, kwa kusema kwamba: "Hataingia Peponi ila aliye Myahudi au Mkristo," na wanamtamani kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu] matamanio mabovu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba wale wanaomuani Mtume wake Muhammad – rehema na amani Mwenyezi Mungu zimshukie – wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwamba wana dhamana mafungu mawili kutoka kwa rehema yake, nuru na msamaha. Hata wasipopenda hivyo Watu wa Kitabu, na kwamba wajue kuwa: "Fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye" miongoni mwa wale ambao hekima yake inahitaji kwamba wapewe katika fadhila zake. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu" ambayo haiwezekani kukadiria kiasi chake.
Imekamilika tafsiri ya [Surat Al-Hadid], na sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu].