الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْمِيزَانَ لِيَقُومَ ٱلنَّاسُ بِٱلْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا ٱلْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَـٰفِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُۥ وَرُسُلَهُۥ بِٱلْغَيْبِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ عَزِيزٌ ٢٥
{25} Anasema Mwenyezi Mungu: "Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ishara waziwazi," ambazo ni ushahidi, hoja na ishara zinazoashiria ukweli wa yale waliyokuja nayo na kwamba ni ya haki. "Na tukateremsha Kitabu pamoja nao." Hili linajumuisha vitabu vyote alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza katika yale yatakayowafaa katika dini yao na dunia yao. "Na mizani" ambayo ni uadilifu katika kauli na vitendo. Na Dini waliyoileta Mitume yote ni uadilifu na usawa katika maamrisho na makatazo, na katika kuamiliana na viumbe, na katika hukumu za jinai, kulipiza kisasi, adhabu maalumu, mirathi na mambo mengineyo, na hayo ni "ili watu wasimamie uadilifu" ili kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, na kufikia masilahi yao, ambayo hayawezi kuyadhibiti wala kuyahesabu. Hili linaashiria kwamba Mitume walikubaliana katika kanuni za asasi za kisheria, ambazo ni kufanya uadilifu, hata kama aina za uadilifu huo zitatofautiana kulingana na nyakati na hali mbalimbali "na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi." Iwe ala ya vita, kama vile silaha, deraya na vitu vinginevyo. "Na manufaa kwa watu" ambayo ni kile kinachoonekana kutokana na manufaa yake katika aina mbalimbali za viwanda, ufundi, vyombo, na mashine za kulima, kiasi kwamba ni mara chache hakuna kitu ambacho hakihitaji chuma. "Na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu." Yaani, ili Mwenyezi Mungu Mtukufu aweke mtihani kwa yale aliyoyateremsha katika Kitabu na chuma, ili ibainike ni nani atamnusuru yeye na Mitume wake katika hali ya ghaibu, ambayo imani ina manufaa ndani yake hata kabla ya kuona kwa macho, ambayo yakishapatikana, hapo imani haisaidii kitu. Kwani wakati huo kuamini kunakuwa ni kitu cha lazima. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda." Yaani, hakuna kinachoweza kumshinda, wala mwenye kukimbia hawezi kumponyoka. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba aliteremsha chuma ambacho hutengeneza kutoka humo vyombo vyenye nguvu. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba ana uwezo wa kuwashinda adui zake. Lakini huwajaribu vipenzi wake kwa maadui wake; ili ajue ni nani atamsaidia kwa ghaibu. Hapa, Mwenyezi Mungu ameiunganisha kati ya Kitabu na chuma. Kwa sababu kwa mambo haya mawili, Mwenyezi Mungu huinusuru Dini yake na kuliinua juu na kulitukuza neno lake kwa Kitabu kuna hoja na ushahidi, na kwa upanga kuna ushindi, Mwenyeezi Mungu akipenda. Na vyote viwili ni vinasimamisha uadilifu na usawa, ambavyo vinatumika kama ushahidi wa hekima ya Muumba na ukamilifu wake na ukamilifu wa sheria yake aliyoiweka juu ya ndimi za Mitume wake.