الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لِّكَيْلَا تَأْسَوْا۟ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا۟ بِمَآ ءَاتَىٰكُمْ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ٢٣
{23} Mwenyezi Mungu aliwajulisha waja wake jambo hili ili kanuni hii ikae imara ndani yao, na wajenge juu yake mema na mabaya yaliyowapata. Basi wasihuzunike kwa yale waliyoyakosa, katika yale ambayo nafsi zao ziliyatamani sana na kuwa na shauku nayo. Kwa sababu wanajua kwamba hilo liliandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, lazima litekelezeke na litokee, na wala hakuna njia ya kulizuia. Na wala wasifurahi kwa aliyowapa Mwenyezi Mungu, kwa furaha ya kiburi na uovu. Kwa sababu wanajua kwamba hawakuipata kwa uwezo wao wala nguvu zao. Bali waliyapata kwa fadhila na neema ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanajishughulisha na kumshukuru yule aliyewapa neema hizo na akawazuilia adhabu, na ndiyo maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha" juu ya neema za Mwenyezi Mungu, akawa anajinasibishia neema hizo mwenyewe, na zikampotoa na kumsahaulisha. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu, husema: 'Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu.' Siyo hivyo! Huo ni mtihani!"