انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

يَوْمَ تَرَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَـٰنِهِم بُشْرَىٰكُمُ ٱلْيَوْمَ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ ١٢

{12} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akieleza fadhila ya Imani na kufurahi kukubwa kwa wana imani Siku ya Kiyama: "Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao." Yaani, ikifika Siku ya Kiyama, na jua likakunjwa na mwezi ukapatwa, na watu wakawa gizani, na ikawekwa Sirat (njia iliyoko) kwenye mgongo wa Jahannamu; basi hapo utawaona Waumini wanaume na Waumini wanawake wana nuru yao mbele yao na kuliani kwao, kisha watatembea kwa nuru yao katika hali hiyo inayotisha sana na ngumu, kila mmoja kulingana na imani yake, na hapo watapewa bishara njema iliyo kubwa zaidi, wakiambiwa: "Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake, mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa." Ee Mwenyezi Mungu, ni bishara njema iliyo nzuri namna gani hii kwenye nyoyo zao, na yenye ladha zaidi kwenye nafsi zao, ambapo walipata kila wanachotafuta, wanachokipenda, na wakaokoka kutokana na kila uovu na kinachohofiwa.