انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الواقعة
السورة ٥٦

الواقعة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٤٥–٤٨

إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ ٤٥ وَكَانُوا۟ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلْحِنثِ ٱلْعَظِيمِ ٤٦ وَكَانُوا۟ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ٤٧ أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ ٤٨

{45 - 48} Kisha akataja vitendo vyao vilivyowapelekea kwenye malipo hayo, akasema: "Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa." Yaani, walidanganywa na dunia yao na wakaifanyia matendo, na wakaifurahia, kwa hivyo matumaini yakawashughulisha mbali na kutenda mema. Hii ndiyo anasa aliyoikashifu Mwenyezi Mungu. "Na walikuwa wakiendelea tu kufanya madhambi makubwa" na wala hawatubii wala kujutia. Bali walikuwa waking'ang'ania kufanya yale yanayomchukiza Mola wao, kwa hiyo wakamjia wakiwa na madhambi mengi yasiyosamehewa. Na pia walikuwa wakipinga suala la kufufuliwa wafu, wakawa wanasema wakilikatalia mbali hilo, "Tutakapokufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? Au baba zetu wa zamani?" Yaani, vipi tutafufuliwa baada ya kufa na kupotelea mbali tukawa udongo na mifupa? Hilo haliwezekani.