الواقعة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ ١٧ بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ١٨ لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ ١٩
{17 - 19} "Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele." Yaani, vijana wawili wadogo wa umri kiume, wazuri sana watawajia mara kwa mara wana Peponi ili kuwahudumia na kukidhi haja zao. "Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa" ambayo haipatwi na chochote kinachoweza kuibadilisha. Nao waliumbwa kwa ajili ya kukaa milele. Hawatazeeka, hawatabadilika wala hata umri wao hautazidi. Nao watawajia mara kwa mara wakiwaletea vyombo vya kinywaji chao. "Kwa vikombe" visivyo na kishikio "na mabirika" zenye kishikio "na bilauri za vinywaji kutoka katika chemichemi safi" vya mvinyo wenye ladha katika kuvinywa na visivyo na madhara. "Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo" baada ya kuvinywa, wala “hawataloweshwa” na kuondolewa akili zao na uelewa wao kwa sababu yake kama ilivyo katika mvinyo wa duniani. Jambo la msingi ni kwamba aina zote za neema zote zilikozo Peponi ambazo mfano wake uko hapa duniani, hazina madhara yoyote huko. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Humo iko mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa mno." Na hapa, akataja pombe ya Peponi, na akasema kwamba haina madhara yoyote kama yale ya duniani.