القمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَكَذَّبُوا۟ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ ٣
{3} Ndiyo maana akasema: "Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao." Kama Asemavyo Mwenyezi Mungu: "Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu." Kwani ikiwa nia yao ingekuwa ni kufuata uwongofu, basi bila ya shaka wangeliamini kabisa na kumfuata Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungi ziwe juu yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaonyesha kupitia mikono yake Nabii ushahidi wa wazi, uthibitisho na hoja za uhakika zilizoonyesha matakwa yote ya kimungu na makusudio ya kisheria; "na kila jambo ni lenye kuthibiti." Yaani, mpaka sasa jambo hilo halijafikia mwisho wake, na jambo hilo litaendelea hadi mwisho wake. Hapo mkweli atakwenda huku na kule katika bustani za mbinguni za neema na msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi zake. Naye mwenye kukadhibisha atapendukapenduka katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake adumu humo milele na milele.