الطور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ ٤٨ وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَـٰرَ ٱلنُّجُومِ ٤٩
{48 - 49} Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozifafanua hoja na ushahidi wa kubatilisha ubatili wa kauli za wanaokadhibisha, alimuamrisha Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – asiwajali hata kidogo, na kwamba asubiri hukumu ya Mola wake Mlezi ya kimipango ya azali ya Mwenyezi Mungu na ya kisheria, kwa kushikamana nazo na kuwa mnyoofu juu yake, na Mwenyezi Mungu akamuahidi kumtosheleza kwa kauli yake: "Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu." Yaani, tunakutazama, na kukulinda na kujali mambo yako, na akamuamrisha kutafuta juu ya msaada kwa kumtaja na kufanya ibada, na akasema: "Na mtakase Mola wako Mlezi unaposimama," [yaani] usiku. Na katika hili kuna amri ya kuswali Swala za usiku, au unaposimama kwenda katika Swala tano za kila siku. Maana hizi zinaashiriwa na kauli yake: "Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota." Yaani, mwisho wa usiku, ambao ni pamoja na sala ya alfajiri. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
Imekamilika tafiri ya Surat At-Tur, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.