الطور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ ٢٩
{29} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuwakumbusha watu, wawe ni Waislamu au makafiri. Ili hoja ya Mwenyezi Mungu isimame juu ya madhalimu, na wale waliowezeshwa waongoke kwa ukumbusho wake, wala asijali maneno ya washirikina wanaokadhibisha, maudhi yao, na maneno yao wanayowazuilia watu kumfuata, ijapokuwa wanajua vyema kwamba yeye ndiye wa mbali zaidi na hayo kati ya watu wote, na ndiyo maana akamkanushia kila upungufu waliokuwa wakimtuhumu nao, na akasema: "Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi si kuhani" ambaye huwa na mwenye kumwangalilia kutoka kwa majini anayemletea habari za ghaibu, kisha akazidisha humo uongo mia moja. "Wala mwendawazimu." Bali wewe ndiye mwenye akili zaidi ya watu wote, wa mbali zaidi na mashetani, mbora wao zaidi katika ukweli, mtukufu wao zaidi na mkamilifu wao zaidi.