انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٣

وَإِذَا سَمِعُوا۟ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا۟ مِنَ ٱلْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكْتُبْنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ ٨٣

{83} Na Miongoni mwake ni kwamba, "wanaposikia yale yaliyoteremshwa" kwa Muhammad - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, - hayo yanaathiri katika nyoyo zao, na wanayanyenyekea, na macho yao yanamiminika machozi kulingana na yale waliyoyasikia ya haki ambayo wana yakini nayo. Basi ndiyo maana, wakaamini na wakaikiri, na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia." Nao ni umma wa Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake; - wanaomshuhudia Mwenyezi Mungu upweke, na kwa Mitume wake kwa utume, na usahihi wa yale waliyokuja nayo. Na wanashuhudia juu ya umma waliopita kwa kusadikisha na kukadhibisha, nao ni waadilifu, ambao ushahidi wao unakubaliwa. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na vivyo hivyo tumewafanya muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu."