المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ٧٦
{76} Yaani, "Sema" ewe Mtume uwaambie, "Je, nyinyi mnamuabudu badala ya Mwenyezi Mungu," miongoni mwa viumbe masikini, wenye uhitaji, ambaye "hawamilikii kudhuru wala kunufaisha." Na mnamwacha Yule ambaye yu peke yake katika kudhuru na kunufaisha, na kupeana, na kuzuia. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia vyema," sauti zote pamoja na kutofautiana kwa lugha mbalimbali, kwa mahitaji mbalimbali; "Mwenye kujua vyema" ya dhahiri na ya siri, ya ghaibu na yanayoshuhudiwa. Na mambo yaliyopita na yajayo; kwa hivyo, Yeye Mkamilifu, Mtukufu, ambaye hizi ndizo sifa zake, ndiye anayestahiki kupwekeshwa katika kila aina za ibada, na kufanyiwa yeye tu Dini.