انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٧

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ بَلِّغْ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ ٱلنَّاسِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ ٦٧

{67} Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Muhammad - swala na salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie, - kwa amri kubwa zaidi na tukufu yake zaidi. Nayo ni kufikisha yale ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia. Na inaingia katika hili kila amri iliyopokewa na Umma kutoka kwake yeye - sala na amani ziwe juu yake – kama vile itikadi, na matendo, na maneno, na hukumu za kisheria, na matakwa ya kimungu. Naye - sala na amani ziwe juu yake – akafikisha kufikisha kukamilifu zaidi, na akalingania, na akaonya, na akabashiri, na akarahisisha, na akawafundisha majahili wasiojua kusoma na kuandika mpaka wakawa katika wanachuoni wachamungu. Na alifikisha kwa maneno yake, na matendo yake, na vitabu vyake, na mitume wake. Na hapakubakia heri isipokuwa aliwaelekeza umma kwayo, wala ovu lolote isipokuwa aliwaonya umma wake juu yake. Na walishuhudia kwamba alifikisha wale walio bora zaidi wa umma huu miongoni mwa Maswahaba na wale waliokuja baada yao miongoni mwa maimamu wa Dini na wanaume Waislamu. "Na usipofanya;" yaani, kama hukufikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi, "basi hujafikisha ujumbe wake." Yaani, utakuwa hujatekeleza amri yake, "Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu." Hii ni kinga na ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutokana na watu, na kwamba inapasa iwe shauku yako juu ya kufundisha na kufikisha, wala isikutishie dhidi ya hilo hofu ya viumbe. Kwani, nywele za upande wa mbele wa vichwa vyao ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Naye alichukua dhamana ya kukuhifadhi. Basi wewe kilicho juu yako kufikisha kwa waziwazi. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, basi ni kwa ajili yake mwenyewe. Na ama makafiri ambao hawana nia isipokuwa kufuata matamanio yao, basi Mwenyezi Mungu hawaongoi, wala hawawezeshi kufanya heri kwa sababu ya ukafiri wao