المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ ٱلْقِرَدَةَ وَٱلْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ ٦٠
{60} Na kwa kuwa kukashifu kwao Waumini kulilazimu kwamba Waumini wako kwenye uovu. Akasema Mwenyezi Mungu, "Sema" ukiwajulisha kuhusu ubaya hali waliyo juu yake. "Je, niwaambie lililo baya zaidi kuliko hilo mlilotukashifu kwalo kwa namna ya kutaka tu kujiweka katika daraja lenu? "Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu alimlaani," yaani, Alimuweka mbali na rehema Yake, "na akamkasirikia," na akamuadhibu katika dunia na Akhera. "Na akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na" [yule "aliyemuabudu Taghuti." Naye ni Shetani, na kila kinachoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu basi hicho ni Taghuti. "Hao" waliotajwa na tabia hizi mbaya "ndio wenye pahali paovu zaidi" kuliko Waumini ambao rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu nao. Na Mwenyezi Mungu amewawia radhi, na atawalipa katika dunia na Akhera. Kwa sababu walimpwekeshea yeye dini. Na aina hii ni katika mlango wa kutumia vitenzi vya kuboresha katika mlango usiokuwa wake. Na vile vile kauli yake, "waliopotea zaidi njia iliyo sawa, yaani, walio mbali zaidi na njia iliyo sawa.