المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَهَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فَأَصْبَحُوا۟ خَـٰسِرِينَ ٥٣
{53} "Na wale walioamini wanasema," kwa kushangazwa na hali ya wale wenye maradhi katika nyoyo zao: "Je, hawa ndio wale walioapa kwa Mwenyezi viapo vyao vikali mno kuwa wao hakika wako pamoja nanyi?" Yaani, waliapa na wakavisisitiza viapo vyao, na wakavifanya kuwa vizito kwa aina mbalimbali za kusisitiza. Kwamba hakika wao wako pamoja nanyi katika imani na yale inayolazimu miongoni mwa msaada, na upendo na kuwafanya marafiki wandani. Lakini yakadhihirika yale waliyoyaficha, na yakabainika yale waliyofanya kuwa siri; na vikawa vitimbi vyao ambavyo walivipanga, na dhana yao ambayo waliidhania Uislamu na watu wake ikawa batili. Kwa hivyo njama zao zikabatilika, vikabatilika "Vitendo vyao" katika dunia, "na wakawa wamehasirika" kwa kuwa walikosa makusudio yao, na wakapatwa na taabu na adhabu.