المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِى مَآ ءَاتَىٰكُمْ ۖ فَٱسْتَبِقُوا۟ ٱلْخَيْرَٰتِ ۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ٤٨
{48} Yeye Mtukufu anasema, "Na tulikuteremshia wewe Kitabu hiki" ambacho ni Qur-ani Tukufu, bora zaidi ya Vitabu, na kitukufu zaidi. "Kwa haki, yaani, kimeteremka kwa haki, hali ya kuwa kimejumuisha haki katika habari zake, na amri zake, na makatazo yake. "Kinachosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Vitabu," kwa sababu kilivishuhudia, na kikakubaliana navyo, na habari zake zikalingana na habari zake, na Sheria zake kubwa zilikuwa ndizo Sheria zake, navyo vilijulisha kukihusu. Kwa hivyo kukawa [kuwepo kwake] ni kwenye kusadikisha habari zake, "na chenye kuyalinda." Yaani, kinajumuisha yale yaliyojumuishwa na vitabu vilivyotangulia, na kuongeza katika matakwa ya kimungu na maadili ya kinafsi. Basi ni kitabu kilichofuatilia kila haki ambayo vitabu vilikuja nayo na vikaiamrisha, na vikaihimiza, na vikazidisha katika njia za kuifikia. Nacho ni kitabu ambacho ndani yake kuna hukumu na hekima, ambacho kiliwekewa vitabu vilivyotangulia mbele yake. Kwa hivyo kile ambacho kinashuhudia kwamba ni ukweli, basi hicho kinakubalika. Na kile ambacho kinashuhudia kuwa kinakatalika, basi hicho kinakatalika, ambacho kimeingiwa na kupotoshwa, na kubadilishwa; na vinginevyo lau kuwa yalitoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hayangekihalifu. "Basi hukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu," katika hukumu ya kisheria ambayo Mwenyezi Mungu alikuteremshia. "Wala usifuate matamanio yao ukaacha haki iliyokujia, yaani, usifanye kufuata matamanio yao machafu, yaliyo kinyume na haki kuwa badala ya haki iliyokujia, basi ukabadilisha kilicho cha chini kwa kilicho bora zaidi. Kwa kila mmoja wenu, enyi umma, tumemwekea "sheria yake na njia yake." yaani, njia na mwenendo. Na sheria hizi ambazo zinatofautiana kwa kutofautiana kwa umma mbalimbali, ndizo zinazobadilika kulingana na mabadiliko ya nyakati na hali; na zote zinarudi kwa uadilifu katika wakati wa kuwa kwake sheria. Na ama misingi mikubwa ambayo ni masilahi na hekima katika kila wakati; basi hiyo haitofautiani. Kwa hivyo inawekwa kama sheria katika sheria zote. "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwafanya nyote umma mmoja." Wenye kufuata sheria moja, wa mwisho wao hawi tofauti na wa kwanza wao. "Lakini ili awajaribu kwa yale aliyowapa." Kwa hivyo atawapa mtihani na aone jinsi mnavyotenda, na ataujaribu kila umma kulingana na kile hekima yake inachotaka. Na atampa kila mmoja kile kinachomfailia, na ili uwepo ushindani kati ya umma mbalimbali. Kila umma ulijitahidi kuwatangulia wengineo. Na ndio maana akasema, "Basi yakimbilieni mambo ya heri." Yaani, yaendeeni haraka na yakamilisheni. Kwa maana heri zinazojumuisha kila faradhi na yale yanayopendekezwa katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, hawi mwenye kulitenda mwenye kumtangulia mwingine mwenye kushinda jambo hilo isipokuwa kwa mambo mawili: Kulikimbilia, na kuichukua fursa muda wake unapofika na alama zake kuonekana, na kujitahidi kuifanya kikamilifu kwa namna ilivyoamriwa. Aya hii inatumika kama hoja juu ya kuharakisha kuswali na mambo mengine katika wakati wake wa mwanzo. Na juu ya kwamba mja anapaswa asiachie tu katika mambo ya faradhi yanayofanyika katika swala na ibada nyinginezo, bali anapaswa afanye mambo yanayopendekezwa ambayo ana uwezo wa kuyafanya ili yatimize na yakamilike na kwayo apate kutangulia. "Kwa Mwenyezi Mungu ndiyo marejeo yenu nyote." Umma waliotangulia na waliofuata baadaye, Mwenyezi Mungu atawakusanya wote kwa Siku isiyo na shaka juu yake, "kisha atawaambia yale mliyokuwa mkihitalifiana juu yake;" ya sheria mbalimbali na matendo. Na awalipe wale wa haki na matendo mema, na awaadhibu wale wa batili na matendo mabaya.