انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٢

سَمَّـٰعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّـٰلُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَآءُوكَ فَٱحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْـًٔا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَٱحْكُم بَيْنَهُم بِٱلْقِسْطِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُقْسِطِينَ ٤٢

{42} "Hao ni wasikilizaji sana wa uongo." Na kusikiliza hapa ni kusikiliza kwa kuitikia. Yaani, kwa sababu ya uchache wa dini yao na akili yao, wanawaitikia mwenye kuwaita kusema uwongo. “Na ni walaji mno vya haramu,” yaani, mali haramu wanazozichukua kutoka kwa watu wao wa chini na watu wa kawaida kwa njia ya taarifa na mishahara isiyo ya haki. Kwa hivyo wakachanganya kati ya kufuata uongo na kula vya haramu. "Basi wakikujia, wahukumu baina yao au wapuuze" kwani, umepewa chaguo katika hayo. Na Aya hii haikufutwa kwani, wakati kundi hili linamtaka kuwa hakimu, anapewa chaguo kati ya kuhukumu baina yao au kuacha kuhukumu kati yao. Kwa sababu wao hawana nia katika hukumu ya kisheria isipokuwa ikiwa inakubaliana na matamanio yao. Na kwa maana hii, Kila mwenye kuuliza na mwenye kutaka hukumu ya mwanachuoni anayejua katika hali yake kwamba, lau atahukumu dhidi yake, hataridhika, basi haitakuwa wajibu wake kuhukumu, wala kuwatolea fatwa. Na akihukumu baina yao, ni lazima ahukumu kwa uadilifu. Na ndiyo maana akasema, "Na ukiwapuuza, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu." Hata kama ni madhalimu na maadui, basi hilo lisikuzuie kufanya uadilifu katika kuhukumu kati yao. Na katika hili kuna ufafanuzi wa ubora wa uadilifu na haki katika kuhukumu kati ya watu, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anaupenda.