انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٢

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَنَّهُۥ مَن قَتَلَ نَفْسًۢا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِى ٱلْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ ٱلنَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَآ أَحْيَا ٱلنَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَآءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِى ٱلْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ ٣٢

{32}Anasema Yeye Mtukufu, "Kwa sababu ya hayo," ambayo tumeitaja katika kisa cha wana wawili wa Adam, na mmoja wao kumuua kaka yake, na kuweka kwake nyendo ya kuua kwa atakayekuja baada yake. Na kwamba kuua mwisho wake ni mbaya, na ni hasara katika dunia na Akhera. "Tuliwaandikia Wana wa Israili." Watu wa Vitabu vya mbinguni "kwamba mwenye kuiua nafsi bila nafsi hiyo kuiua nyingine, au kufanya uharibifu katika nchi," yaani, bila ya haki, "basi ni kama amewaua watu wote." Kwa sababu yeye hana sababu ya kumfanya kutenganisha, na kwamba yeye asikuendee kuua isipokuwa kwa haki. Kwa hivyo alipothubutu kuiua nafsi ambayo haikustahiki kuuawa, Alijua kulingana na yeye kwamba hakuna tofauti kati ya huyu aliyeuawa na wengine, lakini hilo ni kulingana na kile ambacho nafsi yake yenye kuamrisha mabaya inamwita kuyafanya. Kwa hivyo kuthubutu kwake kumuua ni kana kwamba aliwaua watu wote. Na vivyo hivyo mwenye kuiweka hai nafsi, yaani, alimuacha mtu kuwa hai na wala hakumuua pamoja na nafasi yake kumuita amuue, lakini hofu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ikamzuia asimuue. Basi huyu ni kana kwamba aliwaacha watu wote kuwa hai. Kwa sababu yale yaliyomzuia ya hofu yatamzuia kumuua yule ambaye hastahili kuuawa. Na Aya hii iliashiria kuwa kuua kunaruhusika kwa moja ya mambo mawili: Ima aiue nafsi kwa bila ya haki na kwa makusudi katika kufanya hivyo; basi huyu ni halali kumuua ikiwa ni katika wale waliofikia umri wa kujukumika kisheria; aliye sawa na yule ambaye yeye alimuua, ambaye si mzazi wa aliyeuawa. Au akiwa ni mharibifu katika ardhi, kwa kuwaharibia watu dini zao, au miili yao, au mali zao. Kama vile makafiri walioritadi, na wapiganaji na wale wanaolingania uzushi, ambao uovu wao hauwezi kuzuilika isipokuwa kwa kuwaua. Na vile vile majambazi wa barabarani na mfano wao miongoni mwa anayewavamia watu ili kuwaua au kuchukua mali zao. "Na hakika walikwisha wajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi." Ambazo habakii hoja yoyoye baada yake kwa yeyote. "Kisha hakika wengi katika wao," yaani, watu "baada ya hayo" yaani, kubainishiwa kwenye kukata hoja, yenye kulazimu kuwa imara katika ardhi "ni wenye kupita kiasi" katika kutenda maasia na kuwahalifu Mitume ambao walikuja na hoja zilizo wazi.