المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمَا ٱدْخُلُوا۟ عَلَيْهِمُ ٱلْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَـٰلِبُونَ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓا۟ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ٢٣
{23} "Wanaume wawili miongoni mwa wale wanaomhofu" Mwenyezi Mungu Mtukufu, hali ya kuwa wanawatia moyo kaumu yao, wakiwahamasisha juu ya kupigana vita na adui yao na kuikalia nchi yao. "Ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha," kwa kuwawezesha, na neno la haki katika pahali hapa panapohitaji mfano wa maneno yao haya, na akawaneemesha kwa subira na yakini; "Waingilieni mlangoni. Na mtakapowaingilia, basi kwa yakini nyinyi mtashinda." Yaani, hakuna baina yenu na ushindi wenu dhidi yao isipokuwa muwaazimie na muwaingilie mlangoni. Na mkiwaingilia humo, basi watashindwa. Kisha wawili hao wakawaamrisha maandalizi ambayo ndiyo maandalizi ya nguvu zaidi, kwa hivyo wakasema. "Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini." Kwa sababu katika kumtegemea Mwenyezi Mungu, hasa katika mahali hapa, ili kusahilisha jambo hilo na kuwashinda maadui. Na hili liliashiria juu ya ulazima wa kutegemea, na kwamba kulingana na imani ya mja kunakuwa kutegemea kwake.