المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُل لَّا يَسْتَوِى ٱلْخَبِيثُ وَٱلطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ ٱلْخَبِيثِ ۚ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ١٠٠
{100} Yaani, "Sema" uwambie watu kwa kuonya juu ya uovu, na kwa kuhimiza mema. "Sema: Haviwi sawa viovu na vizuri;" katika kila kitu. Basi Imani haiwi sawa na ukafiri, wala utiifu na uasi, wala watu wa Peponi na watu wa Motoni, wala matendo maovu na matendo mazuri, wala mali haramu na mali halali, "hata kama utashangazwa na wingi wa viovu." Kwa maana, hayo hayatamnufaisha mwenyewe kitu, bali yanamdhuru katika dini yake na dunia yake. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, ili mfaulu." Basi akawambia wenye akili za kutosha na maoni kamili. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaongelesha wao, na wao ndio wa kujaliwa na kutarajiwa kuwa na kheri ndani yao. Kisha akajulisha kwamba kufaulu huko kunategemea na uchamungu, ambao ni kuafikiana na Mwenyezi Mungu katika maamrisho yake na makatazo yake. Basi mwenye kumcha, atafaulu kila kufaulu. Na mwenye kuacha kumcha, atapata hasara na atakosa faida.