الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا يَمْلِكُ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلشَّفَـٰعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِٱلْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ٨٦
{86} Na katika utimilifu wa ufalme wake ni kwamba hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyake mwenye mamlaka yoyote juu ya jambo hilo, na hakuna awezaye kumuombea mwingine kwake isipokuwa kwa idhini yake. "Wala hao mnaowaomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu." Yaani: kila aombwaye asiyekuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, Malaika na wengineo hana uwezo wa kuombea, wala hawawezi kuombea wengine isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na wala hawawezi kuombea isipokuwa yule aliyeridhiwa. Ndiyo akasema: "Isipokuwa anayeshuhudia kwa haki" yaani aliyetamka kwa ulimi wake, akikiri kwa moyo wake, akijua anayoyashuhudia, na ni sharti kuwa ushahidi wake huo uwe kwa haki, ambayo ni kushuhudia upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa Mitume wake kwa unabii na utume, na usahihi wa yale aliyoyaleta miongoni mwa misingi ya dini, matawi yake, hakika zake na sheria zake. Hao ndio ambao uombezi wa waombezi unawafaa, na hao ndio watakaosalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kupata thawabu zake.